Skip to main content

Matibabu ya Lissu: Bunge Lamkataa Tena. Soma habari kwa kina hapa!

Spika Ndugai atoa ufafanuzi juu ya matibabu ya Tundu Lissu.

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema utaratibu wa Bunge kugharamia matibabu ya Tundu Lissu unaendelea kufanyiwa kazi na ukikamilika utatolewa ufafanuzi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Jana Alhamisi Aprili 5, 2018 wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni  hapa nchini ikiwa ni siku moja kupita tangu aliporejea nchini akitokea India kwa matibabu.

Mhe Tundu Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7, 2017 na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi ambako alilazwa hadi Januari 6 alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu.

Tangu wakati huo, familia yake na viongozi wa Chadema wamekuwa wakililalamikia Bunge kutogharamia matibabu ya mbunge huyo huku Lissu naye mara kadhaa akizungumzia jambo hilo.

Lakini katika mahojiano hayo aliyofanya na mtangazaji wa televisheni hiyo, Charles Hilary, Ndugai amesema, “Lile tukio (la kushambuliwa Mhe  Tundu Lissu) limekuwa ni jipya, linataka watu wengi waweze kuangalia jinsi ya kufanya. Kwa kifupi kila anayekwenda kutibiwa nje anakuwa na barua ya Wizara ya Afya au kibali kutoka Muhimbili, ndivyo sisi Watanzania tunafanya.”

“Hiyo ni kwa mbunge na asiye mbunge, hata mwananchi wa kawaida utaratibu ndio huo. Sasa kwa mhe Tundu  Lissu alivyotoka Dodoma kila mtu anafahamu alipewa rufaa Nairobi na ndio maana tunaona kwa wabunge wengine wote wanaotibiwa kwa utaratibu huu huwa hawachangiwi hata na Bunge lenyewe", amesema Spika Ndugai. 

Pia Spika Ndugai  amefafanua zaidi kuwa, “lakini Mhe Tundu  Lissu pale pale tulichanga sisi wenyewe wabunge kama wabunge kwa sababu tulikuwa tunajua safari hii ina tatizo ndio maana ikabidi watu wachange kutoka mfukoni.”

Vile vile Spika Ndugai amesema ni sawa na mtu aliyekata rufaa yeye mwenyewe kwenda katika hospitali aliyochagua, “kwa maana ile hakuchagua yeye mheshimiwa Lissu lakini familia yake na chama chake na kadhalika, halijawahi kutokea jambo kama lile katika Bunge letu, lina upya wa aina yake.”

Aidha Spika Ndugai  amesema upya huo unahitaji ushirikiano mkubwa wa familia na Bunge kuweka utaratibu ambao hautakuwa kwa Mhe Tundu  Lissu pekee.

“Hata kesho na keshokutwa huo ndio utakuwa utaratibu utatumika siku zijazo, kwa hiyo bado linafanyiwa kazi siku ya siku litakuja kutolewa maelezo kama linawezekana au haliwezekani.”, amesema Spika Ndugai. 

Kuhusu wabunge kupewa ulinzi baada ya Mhe Tundu  Lissu kushambuliwa, Spika Ndugai amesema Dodoma hali ya ulinzi ni kubwa.

“Dodoma ni salama na tumemwomba kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma wakati wa Bunge na wakati wote ulinzi uwepo na umeimarishwa na sidhani kama litatokea tena,” amesema Spika Ndugai. 

Kwa habari zaidi tembelea http://paulreuben59.blogspot.com

Tuandikie maoni yako au kututumia habari kwa namba hii +255769380126.

Comments

Popular posts from this blog

The court system during colonialism in Tanzania.

Introduction. Pre-colonial Period Administration of justice during this time depended heavily on the social economic and political organization of the society in Tanganyika. Two systems of administration of justice namely; The Centralized and the Non-Centralized systems could be identified at the time. The Centralized Systems was applicable to societies with chiefs who played both roles of adjudicators and that of governors. In the Non-Centralized systems the entire community took part in the adjudication of disputes. However in both systems there were no formalization of procedure in adjudication, the customs of the respective societies prevailed in the process. Colonial Period The German Colonial Period. The Land currently covering Tanzania Main Land, was then included in what was called the German East Africa, it was subjected to the German Colonial Rule from 1886 up to the end of the First Ward War, 1918. During this Germany Colonial Rule the Administration of Justi...

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180, Abiria wote wafariki

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran. Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.  Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani. Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka. Credit: GettyImage " Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko ... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari ambapo Reuters imeripoti. Je tutegemee machafuko zaidi kutokea? Endelea kuwa pamoja nasi bega kwa bega, mshirikishe na mwenz...