Leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha Edward Moringe Sokoine.......Tazama Hapa Alichokiandika Rais Magufuli
Ikiwa leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine aliyefariki dunia Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari, eneo la Dakawa nje Kidogo ya Mji wa Morogoro, Rais Dkt. John Magufuli amefunguka na kueleza alivyomfahamu kiongozi huyo enzi za uhai wake na mchango wake katika Taifa letu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli amesema;
“Katika siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehemu Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi shujaa huyu niliyemjua na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho.
Comments