Je wajua kuwa kuna vitu nane vinavyoharibu uwezo wa ubongo wa binadamu?
Je kuna mda unajisikia kama ubongo wako umeumia au umeboreka?
Kama umejikuta ukiwa katika hali hii na ukaona kuna vitu vingine vya muhimu huvikumbuki kwa urahisi zaidi tena ambavyo umevifanya wewe mwenyewe ujue tayari umeshaanza kupata tatizo la mtindio wa ubongo. Tatizo hili linasababishwa na mambo ambayo tunayafanya kila siku ndio yanayouharibu uwezo wa ubongo wetu.
- Matumizi ya simu au kompyuta yaliyopitiliza.
Kutumia mda mwingi ukiwa unatumia simu mara facebook au Instagram huwa inachukua umakini mkubwa sana ili kutazama picha na video mbalimbali za marafiki na wengine wengi na baadae unajikuta ubongo wako umechoka kwa kuwa umetumika sana bila kuwa na kiasi na baadae unapoteza uwezo wa kufikiria haraka kwa mambo fulani yanayohitajika yafanywe kwa umakini mkubwa zaidi.
2. Matumizi ya vyombo vingi vya habari.
Hii iko sawa na matumizi ya simu au kompyuta yaliyopitiliza, maana kuna watu wanatumia vyombo vingi vya habari na hatima yake ubongo huanza kukonda au afya yake huanza kupotea kidogokidogo. Kwa mfano kutumia TV wakati unatumia simu ni lazima utapunguza kuandika kwenye simu na ubongo kuanza kupoteza uwezo wake maana umeuhusisha na mambo mengi.
3. Kutazama Runinga sana.
Mda ambao unakwenda kuiwasha runinga yako na kuangalia vipindi vya michezo unavyovipenda ubongo wako huwa unaanza kupunguza uwezo wake hasa utakapokuwa unaviangalia kila siku na ubongo utakuwa na tabia hiyo ya kupunguza uwezo wa umakini kila siku hii ikijirudia mara nyingi mtu huyo hujikuta akiharibika sana uwezo wake wa umakini wa ubongo kufikiria mambo mengine ya muhimu.
4. Google.
Hii ni injini tafutaji imejumuisha mambo mengi sana ambayo hayakosekani kulingana na kile unachotafuta.Lakini tunatumia mda mwingi sana kutafuta vitu ambavyo tuna haja navyo kwa mda huo, na matokeo vinakuja vitu vingine tu na tunaanza kuhangaika kutafuta ni kipi uchukue na ni kipi uache hapo ndipo ubongo wetu unapokuwa unachoka kufikiria na kupoteza umakini wake.
5. Kupata mda kidogo wa kulala.
Kulala ni muhimu sana kwa binadamu maana huwa tunahitaji kupumzika na kupambanua mambo tuliyoyafanya na mawazo mbalimbali. Kulala huwa ni muhimu pia kwa sababu ubongo huwa unahitaji kuyapanga mambo ya muhimu na mengine madogo kuyaacha. Kukosa usingizi au kulala uwezo wa ubongo wa binadamu huwa unaanza kuharibika taratibu. Masaa ya kulala kwa mtu mzima ni 7 hadi 8, na mtoto masaa 10 kwa wastani. Sasa kuna wengine wanaolala kwa masaa 6 hadi 5 aidha wakiwa wanachati au wakiwa wanaangalia video na michezo mingine. Kwa wanandoa haijazuiliwa kupumzika kwa starehe lakini tumieni mda wenu vizuri.
6. Vyakula.
Matumizi ya chakula cha sukari nyingi na protini nyingi husababisha ubongo kutokuwa makini na kushindwa kuchagua mambo sahihi lakini pia unaweza kubadilika mpaka muonekano wako wa mwili. Punguza matumizi mengi ya sukari na mayai, nyama au vyakula vilivyo na protini nyingi na sukari.
7. Kuzidisha mda wa mazoezi.
Watu wengi hawafanyi mazoezi nahivyo hupelekea kuwa na matatizo mengi sana ya kiafya lakini wapo ambao hupendelea kufanya mazoezi hadi wanazidisha na hivyo huwa wanapata hamu ya kufanya mazoezi kila mda na hapo ubongo hujenga tabia ya kufikiria jambo hilo kila mda, vijana wengi wanatumia mda wao mwingi kwenda gym mpaka wanaonekana kama vichwa vya habari kwenye magazeti maana hawaondoki, hivyo uwezo ubongo huanza kuharibika kwa njia hii pia.
8. Kuyafikiria sana maisha.
Watu wengi wanafikiria sana kuhusu maisha yao yatakuwaje huko mbele au kwa huo mda yatakuwaje hasa anapoangalia huku na kule anakosa msaada hapo ndipo uwezo wa ubongo huanza kupungua kwa sababu ya kuutumia ubongo sana kufikiria mambo mengi na ulinganishaji mwingi wa maisha yako na ya mwenzako.
Comments