Skip to main content

Posts

Sheria ya kusajili blog yafutwa na Mahakama Kuu Kenya

Mahakama nchini kenya imetupilia mbali sheria mpya ya mitandao ya kutaka vyombo vya habari vya mitandao zikiemo blog kusajiliwa. Chama cha Wanablogu wa Kenya (BAKE) na Umoja wa Kenya wa Waandishi wa Habari (KUJ) kwa mafanikio waliomba rufaa kuzuia sheria hiyo   ambayo ilisainiwa  na Rais Uhuru Kenyatta wiki mbili zilizopita Jumanne, hakimu wa mahakama ya juu Chacha Mwita aliorodhesha vipengele 26 vya sheria hiyo   ambavyo vitaathiri haki na uhuru wa msingi wa kujieleza.  Mkurugenzi wa BAKE James Wamathai alisema: "vipengele hivi vinatakiwa kudhibiti habari za uwongo lakini kwa bahati mbaya hiyo ni kinyume na katiba ... kuna sheria zilizopo za kukabiliana na kesi wakati mtu amelala, hatuhitaji hili." Nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania   zimepitisha sheria ambazo wanaharakati wanalalamika kuzuia uhuru wa kujieleza. Mnamo Aprili, Uganda ilitangaza mipango ya kutoza kodi watumiaji wa vyombo vya habari vya mitandaoni.

Babu Tale Anakabiliwa na Kesi ya Madai ya Mil 250

Mkurugenzi wa Tip Top Connection Hamis Taletale a.k.a Babu Tale ameachiwa huru toka Kituo Kikuu cha Polisi DSM. Tale anakabiliwa na kesi ya madai ya fidia ya shilingi milioni 250 baada ya kushtakiwa kwa kosa la kutumia kazi ya Mhadhiri Sheikh Hashim Mbonde bila ridhaa yake. Kwa habari nyingine bonyeza hapa !

Breaking News! Mwanafunzi Muhimbili Akutwa Amekufa Chumbani Kwake

Hivi Punde: Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Shahada ya Famasia katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Edward Kahitwa amekutwa akiwa amefariki chumbani kwake, chuoni hapo. Afisa Uhusiano wa chuo hicho, Hellen Mtui amethibitisha.

RC MAKONDA APOKEA VIFAA VYENYE THAMANI MILION 400 KWAAJILI YA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Million 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel ltd kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam. Vifaa alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya shilingi Million 360, Nondo Tani 22 zenye thamani ya million 40 ambapo kiwanda hicho kimemuahidi tena kumpatia RC Makonda vifaa vingine ikiwemo Rangi, Nondo na Mabati. Akipokea vifaa hivyo RC Makonda ameshukuru kiwanda cha MMI Steel chini ya mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwasihi wadau na wananchi kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu. Aidha RC Makonda amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture kutoka Marekani, Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii kutoka Marekani, Kontena 10 za vifaa tiba kutoka uingereza na kontena 10 za ...

Jimbo la Mbagala Kutenganishwa-Ofisi ya Rais TAMISEMI

Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeadhimilia kuligawa Jimbo la Mbagala lililopo jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wakazi wanaoishi jimboni humo na kusababisha uhaba wa upatikanaji wa huduma muhimu kutoka kwa Mbunge wao. Soma habari zingine hapa

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ustawishaji Makao Makuu Apandishwa Kizimbani

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Paskas Muragili na mwenzake mmoja wamepandishwa kizimbani kwa kutumia madaraka vibaya. Wanatuhumiwa kutokuweka wazi maslahi yao walipotoa zabuni ya TZS 86.1m kwa Glaciaer Investment