Skip to main content

ABDUL NONDO kushtakiwa mahakamani kwa kudanganya serikali na Umma

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetolea ufafanuzi kuhusu kile kinachoitwa kutekwa kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Nchini TSNP, Abdul Nondo. 


Akizungumza na Wandishi wa Habari Kamanda wa Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mnamo Machi 7, mwaka huu waliletewa taarifa kutoka kwa wenzao wa Iringa ambapo walithibitisha kupatikana kwa mwanafunzi huyo akiwa mzima huku akiwa hajaripoti kituo chochote cha Polisi. 





Mambosasa amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kwa kushirikiana na wenzao wa Iringa walithibitisha kuwa Nondo hakutekwa bali alijiteka ambapo mawasiliano ya jumbe za simu yake zinaonesha kuwa alikuwa akiwasiliana na mpenzi wake aliyepo mkoani humo.



"Kijana huyu ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakutekwa wala kushikiliwa bali alijiteka mwenyewe kwa nia ama ya kutafuta umarufu au kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe", amesema Kamanda Mambosasa. 






"Jeshi la Polisi tunaendelea kutoa onyo kwa sababu hatutomuhurumia mtu yeyote ambaye anatafuta umaarufu kwa kuzua taharuki na wala hatutowapa nafasi ya kuharibu amani ya Nchi," amesema Kamanda Mambosasa.

Comments

Popular posts from this blog

Ndege ya Ukraine yaanguka Iran ikiwa na abiria 180, Abiria wote wafariki

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Watoa huduma wa msalaba mwekundu wa Iran wanasema kuwa hakuna dalili yeyote kama kuna mtu aliyepona katika ajali hiyo. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran. Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.  Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani. Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka. Credit: GettyImage " Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko ... ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari ambapo Reuters imeripoti. Je tutegemee machafuko zaidi kutokea? Endelea kuwa pamoja nasi bega kwa bega, mshirikishe na mwenz...

Constitutional Cases and Administrative Cases in Tanzania

"Fiat Justitia Ruat Caelum" Cases on Constitutional and Administrative Laws in Tanzania By: Reuben Paul List of analysed Cases: (1) Cotwu (T)-Ottu Union and Another. v. Hon. Iddi Simba, Minister of Industries and Trade and 7 Others High Court (Katiti, J.): May 25, 2000 Miscellaneous Civil Cause No. 100 of 1999  (2) Director of Public Prosecutions v. Daudi Pete Court of Appeal (Nyalali C.J., Makame and Ramadhani JJ.A.): Criminal Appeal No. 28 of 1990 May 16, 1991 (3) Hamisi Masisi and Others v. Republic High Court, Miscellaneous Criminal Cause No. 54 of 1978 (4) Julius Ishengoma Francis Ndyanabo v. Attorney General Court of Appeal, Civil Appeal No. 64 of 20 (5) Kukutia Ole Pumbun and Another v. Attorney General and Another Court of Appeal: July 23 , 1993 Civil Appeal No. 32 of 1992 (6) Lausa Alfan Salum and 106 Others v. Minister for Lands, Housing and Urban Development Court of Appeal: November 9, 1994 Civil Appeal No. 15 of 1994 (7) Attorney General v. Lohay Akonaa...