KESHO IJUMAA NI HUKUMU YA KESI YA URAIS KENYA, YALIYOJIRI NI HAYA. Na Bashir Yakub. +255784482959. 1. WAHUSIKA Walalamikaji(petitioners) ni wawili. Wa kwanza Raila Amolo Odinga na wa pili Stephen Kalonzo Musyoka, mgombea mwenza. Walalamikiwa(respondents) ni watatu, wa kwanza ni tume huru ya uchaguzi IEBC. wa pili mwenyekiti wa tume hiyo ndg Wafula Chebukati na watatu ni ndg Uhuru Muigai Kenyatta. Pia kuna walioomba kuingia katika kesi hiyo na kukubaliwa. Wa kwanza mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ameingia kama rafiki wa mahakama(amicus curiae) , wa pili chama cha wanasheria kenya "Law Society of Kenya LSK," nao kama rafiki wa mahakama. Wa tatu na nne ni Dr Ekuru Aukot na Mr. Michael Wainaina ambao wameingia kama wahusika wenye maslahi(interested parties). Hawa nao walikuwa wagombea urais. 2. MUDA WA KESI. Kwa katiba ya Kenya mlalamikaji anazo siku 7 tu za kufungua shauri tokea siku matokeo ...
Usipitwe na Habari za Kila Kona ya Dunia.