DONDOO ZA AFYA........!!!! MAAJABU YA SOYA MWILINI. MAAJABU YA SOYA MWILINI. Soya ni zao la jamii ya mikunde lenye aina nyingi za matumizi; ni zao linalofaa kwa chakula cha binadamu na wanyama na pia ni zao la biashara. Zao hilo lina kiasi kingi cha protini yenye ubora wa hali ya juu kuliko kiasi kilichopo katika aina nyingine ya mazao ya mimea.ZK taasisi inayojishughuliza na uzalishaji wa bidhaa za vyakula lishe na mimea na matunda, vinavyoweza kutiba magonjwa mbalimbali wamezalisha maziwa ya Soya ambayo yana kiasi cha protini inayozidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Hii inamaanisha kuwa maziwa ya soya ni chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini hasa kwa watu wenye kipato kidogo ambao hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama, maziwa na samaki. Aidha, maziwa ya soya yanaa mafuta bora yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol). Uwingi na ubora wa protini katika maziwa ya soya yanaweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuwao...
Comments